March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea CCK achukua fomu ahaidi kuwajengea nyumba wafanyakazi wakiwa kazini

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

Ni Agosti 12,2025,leo Zoezi la Kuchukua Fomu za kugombea nafasi ya kiti cha Rais na Makamo zimeendelea kutolewa katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambapo Mgombea wa kumi toka zoezi hilo lianze  David Mwaijojele kutoka Chama Cha Kijamii(CCK) na mgombea mwenza Masoud Ali Abdalla wamefika kuchukua Fomu hizo ambazo wamekabidhiwa na Mwenyekitiwa Tume hiyo Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua Fomu hizo Mwaijojele amesema kuwa Chama chao kina vipaumbele vingi ambavyo ametaja baadhi kuwa ni mambo ya kilimo cha kisasa,Elimu,Afya na Ajira na kuwajengea nyumba wastaafu wakiwa kazini.

“Tuna vipaumbele vingi ila sasa siyo wakati wa kunadi sera mpaka uteuliwe na Tume ndiyo tutasema vipaumbele vyetu vyote,”amesema.

Aidha amaesema wakishinda wanaenda kushughulikia suala la ajira na wastaafu,”Tumeona mara nyingi wafanyakazi wote waliopo kwenye ajira sasa hivi wanaogopa kustaafu kwasababu ya mazingira.

“Sasa sisi CCK tunamikakati mizuri ya kuwaandalia mazingira mazuri kwa wastaafu ili nyie vijana mchukue hizo nafasi,”amesema.

Ameeleza kwamba mtu anakuwa anafanya kazi hana hata kiwanja hana hata nyumba anawaza akiacha kazi ataishije.

“Sasa tunasema serikali ya CCK kama wananchi wakitupa kuongoza nchi hii tutatengeneza yale mazingira ya kuwakata kodi hao wafanyakazi  na kuwajengea nyumba huku wakiwa wanafanyakazi,”amesema

Pia amesema hivyo hivyo wanamikakati kwa wananchi wakawaida,wafanyabiashara,wajasiriamali wadogo,wachimba migodi,waandishi kuwawekea mazingira mazuri ya kuweka hata mia mia inapofika mwisho wa mwaka CCK itawasapoti kwenye vibanda vyao hata kama ni chumba kimoja .

“Kwahiyo tunamambo mazuri tunasera nzuri,tuna ilani nzuri kuliko zotee kuliko hata ya CCM,”amesema.

Pamoja na hayo aliishukuru INEC kwa mipango iliyopanga na mambo mbalimbali tumekuwa tushirikiana bega kwa bega katika kila hatua .

“Tunashukuru Mwenyekiti,Mkurugenzi na Jopo zima na wafanyakazi wote wa Tume,” amesema.