Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online -Mwanza
Maonesho ya keki Kanda ya Ziwa(Lake zone cake exhibition), yanatarajia kufanyika kwa siku tano kuanzia Septemba 3-7,2025 mkoani Mwanza kwa mara ya kwanza.
Maonesho hayo yamelenga kutoa fursa na kuwakuza zaidi wapishi na wapambaji wa keki pamoja na wauzaji wa vifaa vya keki.
Mmoja wa waandaaji wa maonesho hayo,Magdalena Laizer,amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kujionea na kujifunza vitu mbalimbali kuhusu sekta ya keki.
‘Wananchi waje kwa wingi ili waonje keki, wanunue, wajifunze mengi kuhusu sekta hiyo, wakutane na wadau wa keki Kanda ya Ziwa pamoja na kuburudika kwani hakuna kiingilio,”amesema Laizer.
Amesema,mpaka sasa tayari wadau wa sekta ya keki wamejiorodhesha kushiriki katika maonesho hayo ya kihistoria
“Idadi ya washiriki kujiandikisha inapanda kila siku,kutokana na faida watakazopata ikiwa ni pamoja na mafunzo, kuuza bidhaa, kuonjesha, kupewa tuzo, vyeti, kubadilishana uzoefu, kukutana na wateja wao ana kwa ana, kukua zaidi kibiashara pia kuipa hadhi sekta ya keki nchini,”.
Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamaini maonesho hayo,ambayo yanasaidia kukuza sekta hiyo ya ajira nchini.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI