March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea UMD achukua fomu INEC,ahaidi kusimamia ukusanyaji  kodi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

MWAJUMA Mirambo anakuwa mgombea wa nane kuchukua fomu Tume Hurubya Taifa ya Uchaguzi(INEC) za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha Rais akiwa na mgombea mwenza Mashavu Alawi Haji kutoka Chama cha Union for Multiparty Democracy(UMD).

Mirambo amekabidhiwa mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele jijini hapa leo,Agosti 11,2025.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hizo Mirambo amesema kuwa tukishinda watahakikisha wanasimamia  vizuri Uchumi wa nchi ikiwemo kukusanya kodi vizuri.

“Tunajua serikali kazi yake kubwa ni kukusanya mapato ya kodi,tutahakikisha tunakusanya kodi vizuri ili tuweze kutimiza majukumu ambayo tumejiwekea watanzania waweze kuona raha kuishi kwenye nchi yao,”amesema.

Amesema kuwa UMD wapo tayari kuanza harakati za uchaguzi na wao wanasera  ambazo ni wezeshi kwa watanzania ambazo ni rafiki  na ambazo zitamgusa kila mtanzania katika kuhakikisha wanainua Uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini uchumi wa Taifa kwa ujumla.

“Sisi kama UMD tunaomba watanzania watuunge mkono katika kutupigia kura itakapofika wakati wa kupiga kura kwasababu vipaumbele vyetu ni rafiki kwa kila Mtanzania,Mwanamama,Kijana,Makundi maalum,wafugaji na wakulima.

“Sera za UMD tunaamini katika sera za majimbo katika kuwa na sera za majimbo tunaamini kila Mtanzania pale alipo ataweza kufurahia uchumi uliopo kwenye eneo lake na kwenye Taifa
Hatutajutia watanzania kuzaliwa Tanzania,”amesema.

Aidha amesema kuwa wanajua changamoto za watanzania kuwa ni zile zile ambazo amezitaja,Afya,Elimu,Maji na Miundombinu hivyo wao wakishinda watahakikisha wanzishughulikia ili hata  mtoto anayezaliwa Tanzania aone amezaliwa sehemu sahihi.