Ashura Jumapili,TimesMajira Online-Bukoba,
JMhandisi Johnston Mtasingwa wa TANROADS Kagera,ameibuka kidedea katika kura za maoni za ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jimbo la Bukoba Mjini kwa nafasu ya Ubunge na kuwamwaga wenzake watano kwa kupata kura 1,408 kati ya kura 2958 zilizipigwa na wajumbe.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini,Shaban Mdoe,amesema wagombea walikuwa 5,wajumbe 3033,waliopiga kura 2978,zilizoharibika kura 20 na kula halali ni 2958.
Amesema,wagombea wengine akiwemo Mwalimu Koku Rutha alipata kura 40, Mwalimu Jamila Emilly kura 66,Almasoud Kalmuna kura 640 na Alex Muganyizi kura 804.
Hivyo amemtangaza Mhandisi Mutasingwa kuwa ndiye aliyeongoza kura za maoni sio mshindi kwa sababu mchakato wa chama unaendelea ili kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM kagika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Awali Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Joas Zachwa,amesema mchakato wa kumpata mgombea ubunge bado unaendelea ndani ya chama.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi