Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Mwanza
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imempitisha Ragi Samwel, kuwa miongoni mwa wagombea watano watakaoshiriki mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Ukonga.
Ragi anayejipambanua kwa kaulimbiu ya “Niko Tayari Kuitumikia Ukonga,” sasa ataingia kwenye hatua ya kupigiwa kura na wanachama wa CCM, akitarajia kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Wagombea wengine waliopitishwa kushiriki kwenye mchakato huo ni Jerry Silaa, Vilote Mbele, Rajabu Nyangasa na Alawi Rwegoshora.
Akitangaza majina hayo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA.Amos Makalla, amesema uchambuzi wa majina ulizingatia vigezo vya uadilifu, uwezo wa kiuongozi, na kukubalika kwa wagombea miongoni mwa wananchi wa Ukonga.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI