Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Jeshi la Polis Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia kampeni shirikishi ya utoaji elimu kwa jamii,mwaka huu wamefanikiwa kupunguza ukatili wa kijinsia kwa asilimia 11.46 ikilinganishwa na mwaka 2024 kwa kipindi cha miezi saba kuanzia Januari.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, mara baada ya kupokea spika 10 zinazotembea (movable speakers) kutoka shirika la SOS Children’s Village.

“Mwaka 2024,aliripotiwa makosa ya kubaka 155 na mwaka huu yameripotiwa makosa 135, makosa 19 yamepungua. Makosa ya kuzini na maarimu mwaka huu yameripotiwa matukio 3, mwaka jana yaliripotiwa matukio 5,”amesema DCP. Mutafungwa na kuongeza:
“Makosa mengine yaliyopungua ni pamoja na wizi wa mtoto, ambapo mwaka huu yameripotiwa matukio 2 ikilinganishwa na matukio 5 mwaka jana,matukio ya kutupa mtoto yamepungua kutoka matukio 12 mwaka jana hadi matukio 7 mwaka huu, matukio ya kulawiti yamepungua kutoka matukio 45 mwaka jana hadi hadi matukio 41 mwaka huu,”.
Kaimu Meneja Miradi wa shirika la SOS,Elizabeth Swai, amesema shirika hilo limetoa msaada wa spika 10 zinazotembea, vibao vyenye jumbe mbalimbali na mabango manne,ambapo vitu hivyo vina thamani ya milioni 18 huku lengo likiwa ni kuendeleza elimu kwa jamii na familia.
Amesema,wanaamini katika usalama ndipo amani ya taifa na familia inapopatikana ambayo itasaidia mtoto kufikia malengo.
Kwa upande wake,Kaimu Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza, Godlave Landala, amesema kampeni iliyozinduliwa na Kamanda Mutafungwa imeleta mafanikio kwani imesaidia kuibua matukio mengi ya ukatili yaliyokuwa yanafichwa na mengi yametafutiwa ufumbuzi.
Mafanikio haya ni matokeo ya kampeni iliyofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja, iliyozinduliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa,Aprili 22,2025,Kata ya Kayenze wilayani Ilemela, na kutembelea zaidi ya kata 20 ikiwa na Kauli mbinu isemayo “Mwanza salama, Mtoto salama”.



More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi