March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sumbawanga yatakiwa kutekeleza mpango wa kupunguza vihatarishi vya maafa

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Sumbawanga

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imetakiwa kusimamia na kutekeleza mpango na mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa ulioandaliwa na UNDP,ili uwe chachu ya ushirikishaji jamii na wadau.

Pia kuimarisha mfumo wa utoaji tahadhari ya awali, kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na maafa.

izo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile,mara baada ya kuzindua na kukabidhi nyaraka kwa Halmashauri ya wyilaya ya Sumbawanga, amesema yale yaliyobainishwa kwenye nyaraka hizo ni majanga ya kweli ambayo wanaishi nayo na yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Hivyo amewahimiza wadau wa afya akiwemo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ,kuhakikisha wanafuatilia na kuhamasisha usafi wa mazingira pamoja na watu kutotiririsha maji machafu katika maeneo yao.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa,James Kapenulo,ameishukru ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa pamoja na wafadhili ambao ni Shirika la Maendeleo la Kimataifa Nchini (UNDP) kwa kuendelea kuwajali wananchi pale wanapopatwa na madhira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa,Brigedia Jenerali Hosea Ndagala,amesema lengo la utekeleaji huo ni kuweka mgawanyo wa majukumu kwa wadau wote waliopo katika Wilaya hiyo ili kuweka mikakati endelevu.