Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Dar-es- Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema zaidi ya vikundi 440 kati ya vikundi 945 vilivyoomba mikopo ya asilimia 10, Halmashauri ya jyiji la Dar-es-Salaam vyenye sifa vinatarajia kuanza kupokea fedha Agosti mwaka huu.
Mpogolo,amesema hayo katika kongamano la uelimishaji vikundi juu ya mikopo ya asilimia 10, kupitia mfumo jumuishi,ambapo zaidi ya bilioni 18, zinatolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Amesema utolewaji wa mikopo hiyo kwa vikundi hivyo utakuwa shirikishi na uwazi kwa waombaji na benki zitatoa kulingana na utaratibu mpya,ambao Rais Samia Suluhu Hassan aliruhusu mikopo hiyo kutolewa kwa utaratibu mzuri wa kuomba, kuhakikiwa na kukopeshwa.
Pia amesema awali ukitolewa mkopo wa bilioni 17 kwa sasa Halmashauri imeongeza kiwango hivyo itatoa bilioni 18 kwa wananchi wake ili waweze kukuza uchumi.
Hata hivyo amesema,fedha zinatarajiwa kuongezeka hadi kufikia bilioni 60 kwa miaka miwili, kutokana na marejesho ya mikopo ilivvyo kwenye mzunguko.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Suleiman,amebainisha changamoto zilizojitokeza na kusababisha vikundi vingi kuchelewa kupata mikopo ni biashara ya kikundi kukosa uhalisia wa fedha wanazoomba, uzoefu wa biashara na ukweli.


More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI