Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Sumbawanga
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya,Nyakia Chirukile, amewasisitiza wajumbe wa kamati hiyo,kuwa tayari kabla ya majanga kutokea.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Menejimenti ya Maafa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Chirukil, amesema maafa kama maporomoko ya ardhi, mlipuko wa kipindupindu, radi na ajali za majini yameathiri jamii na uchumi wa wilaya hiyo.

“Kuchukua hatua kabla ya majanga ni nafuu zaidi kuliko kushughulika na athari. Mafunzo haya ni nyenzo ya kuongeza ufanisi wetu katika kuzuia na kukabili majanga,” amesema Chirukile.
Kwa upande wake Kanali Selestine Masalamado kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Maafa, amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022, na yana lengo la kuwawezesha viongozi wa serikali za mitaa kuwa mstari wa mbele wakati wa dharura.

Naye mwakilishi wa UNDP,Clara Peter Maliwa, amepongeza Wilaya ya Sumbawanga kwa kujitoa kikamilifu kushiriki mafunzo hayo na ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha mifumo ya kukabili majanga nchini.
Mafunzo hayo yamewaleta pamoja wajumbe wa Kamati Elekezi ya Maafa ya Wilaya na Kamati ya Wataalamu kutoka Wilaya ya Sumbawanga wakiwa na lengo la kujifunza mbinu bora za kupanga, kukabili, na kurejesha hali baada ya majanga.



More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi