Na Agnes Alcardo,Timesmajira Online
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Julai 19, 2025 jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa Julai 15,2025 katika taarifa ilitolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi,Uenezi na Mafunzo,CPA.Amos Makala,ambapo ameeleza kuwa kikao hicho kitafanyika siku hiyo majira ya saa 4 asubuhi jijini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kitatanguliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inayoendelea kuketi jijini Dodoma, kwa ajili ya kupokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wa Jimbo na Viti Maalumu.
Hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya agenda za kikao cha Kamati Kuu.

More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8