March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dar yatoa Bil 460 kuwezesha makundi maalum ya wajasiriamali

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imetoa jumla ya shilingi bilioni 460.13 kwa ajili ya kuwezesha makundi maalum ya wajasiriamali, ikiwemo wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wamachinga, kwa lengo la kuinua uchumi wa wananchi na kuchochea maendeleo ya biashara ndogondogo jijini humo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayoendlea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Temeke, Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sixtus Mapunda, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa fedha hizo zimewanufaisha vikundi 306 vya wajasiriamali vyenye jumla ya wanachama 2,142, waliotoka kwenye makundi ya wanawake vijanna na wenue ulemavu.

“Kupitia utoaji wa mikopo hii, serikali imeweza kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, pamoja na kundi maalum la wafanyabiashara wadogo – wamachinga,” amesema Mapunda.

Amesema kuwa mikopo hiyo kwa wamachinga, yenye thamani ya 446bn/-, ilitolewa kwa kushirikiana na Benki ya NMB, kwa kutumia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kama dhamana.

 Hili limekuwa suluhisho muhimu katika kuwawezesha wamachinga kupata mitaji ya kuanzisha na kukuza biashara zao.

“Kupitia dhamana ya vitambulisho vyao, wamachinga sasa wamepata fursa ya kupata mikopo rasmi. Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya serikali na sekta ya fedha katika kujenga uchumi wa watu,” ameongeza.

Kwa mujibu wa Mapunda, mikopo ya mwaka wa fedha 2024/2025 iliyotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Kinondoni  5.1bn/- Temeke 4.6 bn//- Ubungo 2.02bn/- Jiji la Dar es Salaam  1.7 bn/- na Kigamboni  669.3m/- 

Mapunda amesema mikopo hiyo imechangia kuanzishwa kwa miradi mbalimbali ya kiuchumi, ikiwemo biashara za uzalishaji, huduma, na ubunifu, ambayo inachochea ujasiriamali na kukuza vipaji vya vijana.

Ametoa wito kwa wawekezaji kutumia fursa za uwekezaji zilizopo mkoa wa Dar esalaam katika sector mbali kama za. Kilimo, ufuhaji, uvuvi, utalii, michezo usafirishaji nak.

 Nialike wawekezaji kuja kuwkeza Dar es salama kwani mazingira ni  salama,” amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade,Latifa Khamis amesema siku ya Dar es Salaam  inawasaidia kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali.

“Siku hii ni muhimu kwa watu wa Dar es Salaam kukutana na wadau mbalimbali ambao wanaweza kuzungumza na kubadilishana mawazo katika kuongeza ufanisi wao kwenye maeneo mbalimbali,”amesema