Na Irene Clement,Timemsmajira online
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Leonard Akwilapo, amesema TEA itaendelea kufadhili miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya mafunzo ya amali katika shule na vyuo mbalimbali nchini, ili kuimarisha elimu ya vitendo na kuwajengea vijana ujuzi wa kujitegemea.
Dkt ametoa kauli hiyo alipotembelea Banda la TEA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema TEA imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amali kwa ajili ya kuwezesha utoaji bora wa elimu hiyo nchini.
“Fedha za kutosha zimepatikana kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo katika shule zilizoteuliwa kutoa mafunzo ya amali tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia TEA fedha kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa”amesema.
Vilevile, Dkt. Akwilapo alizungumzia utekelezaji wa Mradi wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na kusimamiwa na TEA, ambao umewawezesha vijana kupata mafunzo yanayowawezesha kujiajiri na kujipatia kipato.
TEA imeshiriki Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake, pamoja na kujenga mahusiano na wadau muhimu ili kuimarisha shughuli za kazi

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi