Na Bakari Lulela,Timesmajira
NAIBU waziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ameipongeza sekta ya Nishati kwa kuendelea kutoa huduma bora ya upatikana wa umeme kwa watanzania.
Akizungumza jijini Dar es salaam, kwenye kituo cha kupoozea umeme cha kinyerezi Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko amesema uboreshaji huu ni chachu ya maendeleo kwa watanzania.
“Hatua ya kwanza ni uboreshaji wa miundombinu ya umeme kwa wananchi lakini pamoja na hilo ni kuweza kuufikisha umeme kwa watumiaji wa mwisho,” amesema Biteko
Aidha Biteko amelipongeza shirika la umeme la Tanesco kwa uwajibikaji wake wenye uweledi na kuwa na wafanyakazi wenye kujituma katika kuweka Tanzania kwenye upatikanaji wa huduma bora ya Nishati kwa jamii.
Hata hivyo Dkt. Biteko amesema kuwa awali nchi yetu ilikuwa kwenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Nishati hususani katika mkoa wa Dar es salaam kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo kigamboni , kinyerezi,mbagala na Gongo la mboto ambapo kumekuwa na maboresho mbalimbali.

Ameendelea kusema kuwa katika bajeti ya mwaka uliopota sekta ya Nishati ilipatiwa fedha za kutosha kama kiasi cha zaidi ya trilioni 2.3 kwa ajili ya kuendeleza sekta ya umeme nchini.
Kulingana na maboresho ya umeme shirika la umeme Tanesco limeboresha huduma maeneo ya kinyerezi kutoka ukubwa wa trasfoma 250 na kuongeza trasfoma mbili zenye ukubwa wa 175 za umeme.
Naibu huyo amesema kuwa kwenye chanzo cha upatikanaji wa huduma kwenye bwawa la mwalimu Nyerere ujumla ya megawati 1000 kimeweza kupatikana na kuongeza tija na ufanisi kwa wateja.

Kwa pande wake mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kuwa hizo zote ni jitihata za serikali ya awamu sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na maendeleo katika sekta ya Nishati.
Sambamba na Hilo amemshukuru Rais na Naibu Waziri na kuwataka kila la heri katika majukumu mbalimbali ya kitaifa na kuwahimiza wawekezaji kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi