Na Heri Shaaban
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Upanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sulitan Salim amesema akichaguliwa kuwa Diwani wa kata hiyo ataifanya kuwa ya kisasa zaidi.
Sultani aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kuomba kura kwa wananchi wake ili waweze kumchagua katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Alisema akipata ridhaa ya wananchi, kata hiyo itajengwa upya chini ya mradi wa UDMP katika kuboresha miundombinu na makazi ya watu.
Pia aliwataka wakazi wa kata hiyo kumpigia kura mgombea wa nafasi ya Urais, Dkt. John Magufuli na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, ili waibuke kwa kishindo waweze kuleta maendeleo.
Alisema CCM ndiyo chama kinachotekeleza Ilani yake na yeye kama atachaguliwa atatekeleza yote yaliyoelekezwa katika Ilani hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Raiymond Mwangala alisema Dar es Salaam itakuwa kitovu cha biashara.
More Stories
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini