Na Bakari Lulela, Timesmajira Online-Dodoma
BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCongo) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu,limeandaa kongamano la mwaka ambalo litafanyika kuanzia Agoust 11 hadi 13,2025, katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Kauli mbinu ya kongamano hilo ni tathmini ya miaka mitano ya mchango wa Mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya Taifa: mafanikio, changamoto fursa na matarajio ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCongo),Jasper Makala amesema katika kongamano hilo wanategemea kupata washiriki zaidi ya 2000 kutoka ndani na nje ya Tanzania ambao wataungana nao katika tukio hilo.
“Kama sehemu ya maandalizi ya kongamano hili kumekuwa na majukwaa ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ngazi za wilaya na mikoa ambayo yamefanyika na mengine yanaendelea kufanyika,” amesema Makala
Makala amesema wageni rasmi kwenye majukwa ngazi za wilaya na mikoa ni Wakuu wa Wilaya zote 103 na Wakuu wa mikoa 14, ambao wamefanikisha majukwaa.
Kwa upande wake Meneja Kitengo cha Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Stanbic Bank Tanzania Limited,Naomi Luze,amesema kuwa benki hiyo imekuwa mdau mkubwa katika kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu katika kutekeleza majukumu yake.
Hata hivyo wakiwa wanamaliza miaka 30 nchini Tanzania,wanaendelea kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuwawezesha kupata huduma bora za kifedha ili kuwahudumia watanzania kwa ufanisi zaidi.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI