Na Bakari Lulela ,Timesmajira
DIWANI mstaafu wa kata ya mtoni na kada wa chama cha Mapindizi (CCM) mh Bernard Mwakyembe Leo ni siku muhimu kwake akirejesha fomu ya kugombea kiti cha ubunge katika Jimbo la Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini na waandishi wa habari wakati akirejesha fomu mgombea huyo amesema kuwa wengi watastaajabu kwanini amegombea kiti hicho cha ubunge ilihali mwaka 2020 aliwahi kuwa kampeni meneja wa mbunge wa Temeke.
“Kimsingi uchaguzi huchukua muda wa miaka mitano hivyo Dada Rose amefanya yaliyo ya kwake na amemaliza na sasa naingia Mimi nifanye yanayostahiki kuyafanya naomba mungu anijaalie,” amesema Mwakyembe
Aidha mgombea huyo ametaja vipaumbele vyake endapo akipata ridhaa ya kuchaguliwa ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya Barabara, masoko na kuhakikisha vijana wanapata fursa za ajira zilizo rasmi.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro