Na Yusuph Mussa, Lushoto
Msisimko na mvutano kwenye Jimbo la Mlalo mkoani Tanga umezidi kuongezeka baada ya mwanachama mwingine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gao Ngwilizi kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, mwaka huu.
Ngwilizi ambaye ni mtoto wa mwanasiasa nguli kwenye Milima ya Usambara na Tanzania, Hayati Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, amerudisha fomu hiyo leo Julai 2, 2025 kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Lushoto.
Ngwilizi anaungana na baadhi ya wanaCCM wengine kwenye kinyang’anyiro hicho Jimbo la Mlalo akiwemo Amiri Mkufya na Mbunge wa sasa Rashid Shangazi.
Kwa Jimbo la Lushoto, baadhi ya waliochukua fomu na kurudisha ni aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mathew Mbaruku, Dkt. Wemael Chamshama, Wakili msomi Remigius Mainde, Hellen Mushi na Mbunge wa sasa Shaaban Shekilindi.
Kwa Jimbo la Bumbuli, ukiacha Mbunge wa sasa January Makamba, baadhi ya waliochukua fomu ni Hussein Mshangama.
MWISHO.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi