Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining), Peter Mashili ametangaza nia ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini.
Huku akiahidi kumng’oa Mbunge aliyepo, Hussein Bashe ambaye ni Waziri wa Kilimo kwa madai kwamba anastahili kupumzika baada ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka kumi.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nzega, Peter Mashili amesema kuwa ameamua kugombea Ubunge kwa sababu wananchi wa Nzega wanahitaji nguvu na kasi mpya, ili kuendeleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano 2025-2030.
Amesema akiteuliwa na chama hicho kwenye mchakato wa kura za maoni kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini,atajikita zaidi katika ushirikishwaji wa wananchi kwenye mambo ya msingi ya maendeleo endelevu, kuwasemea wananchi Changamoto zinaowakabili, kuwapambania ili wanufaike na Fursa zinazotolewa na Serikali hasa katika uendelevu wa sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kwa lengo la Kukuza kipato kwa wananchi ili wajiendeleze kiuchumi na kukuza pato la Taifa.
Peter Mashili ambaye ni mbobezi katika uchimbaji na uuzaji wa madini ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mbugani katika Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ni miongoni mwa wafanyabiashara mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania ambao wana historia kubwa katika ushiriki wa shughuli za kijamii hususani uboreshaji wa miundombinu ya elimu.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako