*Kwa ajili ya kuleta haki, amani na mshikamo kwa jamii.
*CCM yawatakia watanzania wote heri ya kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu leo
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM) kinatoa salamu za heri na baraka kwa waislamu wote nchini na duniani kote katika kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu 1447 muharram.
Akitoa salamu kwa niaba ya chama hicho, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema mwaka huu mpya wa kiislamu ni fursa kwa wauminu wa duni hiyo kutafakari maisha ya Mtume Muhammad ( S. A. W), hususani ujasiri wake, uvumilivu na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kuleta haki, amani na mshikamo kwa jamii.
” Kwa niaba ya CCM na kwangu binafsi nawatakia waislamu wote mwaka mpya uliojaa mafanikio, afya nje, amani na mshikamano.Tunathamini mchango wa jamii ya kiislamu katika kujenga taifa letu, kukuza maadili, kuimarisha uzalendo na kudumisha utaifa”, amesema Balozi Nchimbi.
Aidha ametoa wito kwa watanzania wote, bila kujali tofauti za kidini, kuuenzi mwaka huu kwa kudumisha misingi ya mshikamano wa kitaifa, kuvumiliana na kushirikiana katika kujenga taifa katika misingi ya haki na maendeleo endelevu.
Hata hivyo amesisitiza kuwa chama hicho dhamira yake ni kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa nchi ya amani, umoja na maendeleo kwa wote.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako