mwandishi: Ismail Mayumba
Kauli inayozungumzwa sana kwa sasa nchini Tanzania ni “No Reforms, No Election”, kauli ambayo pia imeenea katika nchi jirani kama Kenya na Uganda. Itikadi hii ilianzishwa na chama cha upinzani CHADEMA, kikidai kuwa kunahitajika kufanyika mabadiliko ya kisiasa na kisheria kabla ya wao kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
Hisia kuhusu kauli hii zimekuwa nyingi na zenye mitazamo tofauti. Hata hivyo, mijadala mingi imehamia kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, ambako hashtag ya #NoReformsNoElection imekuwa ikitawala katika sehemu ya maoni (comments). Watumiaji wengi wa Instagram wamekuwa wakiandika maoni yenye hashtag hiyo kwenye kurasa za watu maarufu wa Kitanzania, bila kujali maudhui ya machapisho hayo.
Wapo wanaokerwa na hali hiyo, huku wengine wakifurahia kwa kuona ni njia ya kuonesha msimamo wao wa kisiasa. Baadhi ya watu wameanza kuogopa kuchapisha maudhui yao kutokana na maoni mengi ya #NoReformsNoElection. Hali hii imeathiri kwa kiasi fulani watayarishaji wa maudhui mtandaoni, japo wapo wengine wanaoendelea kuunga mkono kampeni hiyo kwa kueneza maudhui yenye ujumbe huo.

Instagram ina kipengele kinachokuwezesha kuzima maoni yenye maneno au alama maalum kama vile #NoReformsNoElection. Ili kufanya hivyo, nenda kwenye wasifu (profile) wako, kisha bofya menyu iliyo juu ya ukurasa. Katika menyu hiyo, andika “Hidden Words” kwenye kisanduku cha utafutaji. Ukishaingia hapo, utaweza kuandika maneno au alama ambazo hutaki zionekane kwenye maoni ya machapisho yako. Hivyo, kama hutaki kuona maoni yenye kauli au hashtag ya “#NoReformsNoElection”, unaweza kuyaandika maneno hayo kwenye sehemu husika na hata kama watu wengi wakitoa maoni yenye kauli hiyo, hayatakuonekana kwenye maudhui yako.
Hii ni njia mojawapo ya kulinda amani na kuhakikisha kuwa maudhui yako yanaendelea kufikiwa kwa utulivu

More Stories
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria