Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Ilala
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imetenga kiasi cha bilioni 18,kwa ajili ya mkopo wa asilimia 10, inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo,katika kongamano la Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam, amesema fedha hizo zitakopeshwa kwa vikundi vya wajasiriamali vilivyosajiliwa na kutimiza taratibu za kukopa vilivyopo wilayani Ilala.

Mpogolo, amesema jumla ya vikundi 940 mpaka sasa vimeishaomba mkopo huo wa asilimia 10, hivyo halmashauri hiyo imejipanga kuanza kutoa fedha hizo.
Pia amewataka wajasiriamali wadogo wa wilaya hiyo kukaa mkao wa kupokea fedha kupitia taasisi za benki ambazo zimepewa jukumu la kuwakopesha.
“Vikundi vyote vilivyotimiza taratibu kutoka Jimbo la Segerea, Ilala na Ukonga vyote vitapewa fedha, ili kukuza uchumi wa nchi yetu,”.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam,Elihuruma Maberya,amesema utaratibu wa mikopo kwa sasa ngazi ya Halmashauri wanatoa benki na kabla ya kukopa lazima wakuhakiki.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako