Na Mary Margwe, Timesmajira Online-Simanjiro
Katika kipindi cha miaka mitano Serikali imepeleka zaidi ya bilioni 10.5,kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Diwani wa Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Lucas Chumba,akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kitongoji cha Endiamtu, amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha 2020-2025, Serikali ilipeleka fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo.

Chimba amesema,mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi la ‘Tanzanite City’ ( soko la madini ya Tanzanite) wenye thamani ya bilioni 5.4, unaendelea kwenye Kata hiyo.
Mradi mwingine ni wa maji wenye thamani ya zaidi ya bilioni 4.3, afya milioni 300.6 na sekta ya elimu msingi na sekondari wenye zaidi ya milioni 500.
Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo, Aponary Massawe amesema, katika kipindi hicho cha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kupitia Diwani huyo Kata hiyo imeweza kupata maendeleoabalimbali ikilinganishwa na kipindi kilichopita.
Huku akitolea mfano jitihada alizofanya Diwani huyo Ikiwa ni pamoja na kutengeneza madawati 87 yenye thamani ya milioni 6.96, hali iliosaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati.

Naye Salama Rajabu amesema, ujenzi unaoendelea wa jengo la soko la madini ya Tanzanite utakapokamilika wananchi wataweza kubadilisha maisha yao kupitia uwekezaji wake katika kufanya biashara mbalimbali za ujasiliamali na kujiongezea kipato.
More Stories
WMA yafikia asilimia 96 utekelezaji mpango kazi wa Mwaka
Kamishna wa umeme na nishati jadidifu afanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme jijini Dar
Majaliwa:Wanufaikaji Mikopo ya Elimu ya Juu kuongezeka