June 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jela maisha kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka mitatu

Ashura Jumapili,TimesMajira online Kagera.

Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imemuhukumu kifungo cha maisha Valentine Buberwa alimaarufu Baba Mzazi mwenye umri wa miaka ( 41 ),kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.

Wakili wa serikali Amon Mang’era wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,amesema kuwa kesi hiyo ilianza kusikilizwa Oktoba 25,2024.

Mange’ra, amesema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wanne.Hivyo baada ya mahakama kusikiliza ushahidi uliotolewa pande zote mbili bila kuacha shaka yoyote, ilimtia hatiani Valentine kwa kosa la kubaka kinyume na kanuni ya Adhabu kifungu cha 131 kifungu kidogo cha ( 3) sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022 na kumfunga kifungo cha maisha.

Hukumu hiyo imetolewa ambapo jukumu hiyo ilitolewa Mei 30,2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Frola Kaijage, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Pia amesema mazingira yalikotendewa kosa hilo ni kuwa muathurika wa tukio hilo akiwa na ndugu zake wawili mmoja mwenye umri wa miaka ( 6 )na mwingine miaka ( 14 )walikuwa maeneo ya nyumbani kwako,ambapo Valentine ambaye kwa sasa ni mfungwa akamchukua mtoto huyo na kumuingiza ndani kwake alipokuwa anaishi pekee yake akamfanyia kitendo cha ubakaji.

Ndugu wa mtoto huyo waligundua kutokuwepo kwake katika sehemu aliokuwa amekaa mwezao,ndipo wakaamua kuchungulia kwenye nyumba ya jirani kupitia uwazi uliokuwa kwenye dirisha la nyumba hiyo,ndipo walipomuona Valentine,akimfanyia kitendo hicho ndugu yao hivyo wakachukuanhatua ya kutoa taarifa kwa fami

Awali Mang’era,amedai kuwa kosa hilo lilifanyika Septemba 14,2024 na baada ya taarifa kutolewa mtuhumiwa alikamatwa siku hiyo hiyo na mtoto alipatiwa matibabu na kesi ilifunguliwa mahakamani.

Sanjari na hayo Wakili wa serikali Amoni Mang’era, amesema Mahakama ya Wilaya ya Bukoba imemuhukumu mfanyabiashara wa samaki Abdul Suleiman mwenye umri wa miaka ( 30 ) kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka ( 7 ).

Mang’era,amesema kesi hiyo ilianza kusikilizwa Agousti 14,2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Frola Kaijage na kudai kuwa tukio hilo la kubaka lilitokea kati ya Aprili na Mei, 2024.

Amesema mazingira ya kosa ni kwamba muathurika wa tukio hilo alikuwa anaenda shule,njiani alikutana na mshitakiwa ambaye kwa sasa ni mfungwa,ambaye alimchukua na kumpeleka mazingira ambayo inasemekana kuna jumba bovu na kuanza kumbaka humo zaidi ya mara moja kwa siku tatu mfululizo.

Baada ya mahakama kuridhika na ushahidi ulitolewa na upenda wa mashtaka bila kuacha shaka yoyote,Mei 28,2025 ilimtia hatiani mshitaliwa kwa kumfunga kifungo cha maisha kwa kutumia kanuni ya Adhabu kifungu cha 131 kifungu kidogo cha ( 3 )sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.