May 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAZAMA PIPELINE yalishika mkono jeshi la polisi Mbeya

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limepokea pikipiki mbili aina Boxer kutoka kwa kampuni ya TAZAMA PIPELINE ikiwa ni sehemu ya kutambua jitihada za jeshi hilo katika ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Akikabidhi pikipiki hizo,Mkuu wa Rasilimali watu wa kampuni ya TAZAMA PIPELINE, Greatus Nsemwa, amesema lengo la kutoa pikipiki hizo ni kuongeza nguvu katika ulinzi na usalama mkoani Mbeya.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benjamin Kuzaga,ameahidi kuwa pikipiki hizo zitasaidia kuimarisha usalama na kusaidia askari kufika kwa urahisi maeneo ya kazi.

Naye, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya Mrakibu wa Polisi (SP) Notker Kilewa, amesema kuwa jeshi hilo litaendelea na utaratibu wa kupishanisha magari makubwa na madogo maeneo ya mlima Iwambi na Inyala ili kupunguza madhara yasitokee pindi ajali inapotokea.

Pia, amesema kupitia kikosi cha usalama barabarani wanaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali ikiwemo kuwafungia leseni, kuwapiga faini na kuwafikisha mahakamani.