March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ulega:Mafundi sanifu kujengewa uwezo

Na Bakari Lulela,Timesmajira

WAZIRI wa ujenzi Abdallah ulega ameagiza bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) kuongeza Juhudi za kusajili wataalamu wa kada ya mafundi na kuwajengea uwezo ambapo idadi iliyopo sasa hailingani na ile wanaostahili kuajiliwa.

Waziri ulega alitoa agizo hilo mei 22,2025 Mkoani Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya saba ya mafundi sanifu ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali.
tu.

“Wizara yangu kwa kushirikiana bodi ya usajili imeanza mchakato wa kupata mifumo ya ARB ambapo jumla ya mafundi sanifu waliosajiliwa ni 3000 tu,” amesema Ulega

Aidha Ulega amesema sote tunafahamu kazi ya uboreshaji uchumi hatuna budi kuongeza mafundi sanifu kwa lengo la kuongeza wigo wa wajuzi katika fani ya ufundi sanifu katika .

Serikali ya swami ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani imeendelea kuboresha miundombinu ya kikazi kwa manufaa ya nchi yetu.

Hata hivyo mafundi sanifu ni kioo cha maendeleo hivyo tunatambua changamoto zenu ikiwemo upandaji wa vyeo pia Kuna mchakato madhubuti ya kufahamu uhalali wa mafundi sanifu kwa maendeleo ya nchi yetu.