May 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kongamano la kimataifa la kusoma Qur’an kufanyika Mei 24,2025

Na Hadija Bagasha,Timesmajira Online,Tanga,

BARAZA la Masheikh mkoani Tanga, limeandaa kongamano la kimataifa la kusoma Qur’an(Tawhid),huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sharifu Ahmad ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ushirikiano wa Masheikh mkoani Tanga, amesema kongamano hilo litafanyika Mei 24 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Sharifu,amesema kongamano hilo litajumuisha wasoma Qur’an 13,000,kutoka ndani na nje ya Tanzania, watakaoshindana kusoma Tawhid.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya TAMTA Shamsiyah, Mohamed Dhikiri,amesema kongamano hilo litaanza kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana.

Naibu Mudir wa taasisi ya Shamsiyah Sheikh Ramani Mabruk,amesema umuhimu wa kongamano hilo ni kuwaunganisha watu ili wawe kitu kimoja.Pia litakuwa na faida kwa jamii.

Mudir wa taasisi ya Kiislamu ya Ali bin Abi Talib, Sheikh Mohamed Zuber,amewaomba waislamu na wasiokuwa waislamu kuhudhuria kwa wingi kongamano hilo ambalo pia litatumika kuombea amani ya nchi na viongozi wake.

Amesema washiriki wa kusoma Qur’an watatoka nchi za Pakistan, Uingereza na sehemu nyingine za duniani.