Na Joyce Kasiki,Dodoma
MBUNGE wa Arumeru Mashariki Dkt.John Pallangyo amehoji kuhusu kusuasua kwa mradi wa maji katika kata za Majani ya Chai,Katiti hadi Samaria kata ya Maroroni .
Akiuliza swali Leo Mei 16 Bungeni jijini Dodoma Mbunge huyo amesema mradi huo unatekelezwa kwa kusuasua ambapo baada ya kufuatilia amegundua mkandarasi ndiye mwenye matatizo.
Kufuatia hali hiyo amesema ipo haja ya kuchukua hatua Ili mradi huo utekelezwe kwa kasi inayotakiwa.
“Mradi wa maji wa unaogusa kata za Maji ya Chai,Katiti hadi Samaria kata ya Maroroni unatekelezwa kwa kusuasua sana ,na katika ufuatiliaji wangu nimegundua kwamba mkandarasi ndiye mwenye matatizo kwa hiyo Kuna haja ya kuchukua hatua stahiki ,je Waziri utakuwa tayari kuongozana na Mimi twende jimboni tukafanye Mkutano eneo la tukio tukiwa na Wadau wote akiwemo Mkuu wa wilaya,Mbunge mwenyewe na Wakala wa Maji Mjini na Vijijini (RUWASA)?”amehoji Pallangyo
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Wizara ya Maji,Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amemtoa hofu Mbunge huyo kuhusu utendaji kazi wa mkandarasi huku akisema kwa kuwa anafanya kazi kwa Mkataba husika,suala hilo litafanyiwa kazi.
“Mkandarasi yeyote ambaye hatekelezi majukumu yake, anafahamu namna Sheria ambavyo zinambana ,kwa hiyo nikutoe hofu Mheshimiwa Mbunge,naamini Wizara ya Maji wataenda kushughulikia na kuona kwamba anafika eneo la kazi na kufanya kazi yake “amesema Mhandisi Mahundi
Kuhusu kwenda Jimboni Mhandisi Mahundi amesema ,suala hilo atalifikisha kwa Waziri husika ambalo anaamini atalifanyia kazi kama ilivyoombwa na Mbunge Pallangyo .
More Stories
Kiongozi wa Mwenge awataka RUWASA kukamilisha mradi wa maji kwa wakati Kilindi
Balozi Nchimbi aongoza waombolezaji kumuaga Mzee Mongella
Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mama yake mzazi