Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
IMEELEZWA kuwa uwepo wa mashindano ya Tulia Marathoni Jijini Mbeya umekuwa na mwitikio mkubwa kwa jamii na hivyo manufaa yake kuonekana kwa wajasiliamali ambao wanajishughulisha na biashara mbalimbali za kujiingizia kipato.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Raphael Group Limited, Raphael Ndelwa mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Tulia Marathoni ambayo yamefanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Ndelwa amesema kwamba mashindano hayo yamekuwa fursa ya namna ya kukutana wana Mbeya na kuwa kumekuwa hakuna ya kukutana kwenye matukio makubwa ya kuwakusanya na kuwa kwa eneo moja lakini mashindano hayo yanafanya kuwakutanisha na watu wengi.

“Lakini tukio hili limekuwa likitufanya kukutana na watu wengi wakiwemo wafanyabiashara,wanasiasa,wanamichezo, wafanyakazi hivyo wote tunakuwa tunafanya tukio moja kwa wakati mmoja ,pia naona kuna faida.kubwa katika mashindano haya vijana wetu wanaoshindana wanapata fedha ambazo zinawasaidia kuendesha maisha yao “amesema Mkurugenzi huyo .
Akielezea kuhusu toka kuanzishwa kwa mashindano hayo , Ndelwa amesema kuwa amekuwa akishiriki kila mwaka na mpaka Sasa ni mwaka wa tisa na kwamba kila mwaka yamekuwa yakiendelea kuwa makubwa kuliko yalivyo sasa.
Akizungumzia kuhusu kuboresha mashindano hayo amtaka wananchi waone kuwa sio ya wageni bali ni ya wana Mbeya wote hata kama hawajaweza kuchangia wafike na kujumuika na vikundi mbalimbali ili kukutana na watu wa tofauti”amesema Mkurugenzi huyo.
Kuhusiana na watoto wanaposhirikishwa kwenye mashindano wanaendelea kuwakumbusha wazazi umuhimu wa michezo na wao wataendelea kuwa na kumbukumbu hivyo kitakuwa ni kizazi ambacho kinajengwa kupenda michezo ya namna hiyo,kadri wanavyokuwa wanaweza kufanikiwa na kutoa sapoti.
“Mimi nimeshiriki toka mwaka wa kwanza mpaka sasa mwaka wa tisa kitu kinanifanya nishiriki ni kusikia na kupata kile ninachotaka katika moyo wangu ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali hapa wapo watu kutoka mikoa tofauti tofauti mimi nimejifunza vitu vingi kila ninaposhiriki kumekuwa na mabadiliko makubwa sanaa ,miaka inayofuata kutakuwa na udhamini mkubwa zaidi ya hapa”amesema Ndelwa.
Fred Mwakibete ni Mbunge wa Busokelo mkoani Mbeya ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika mashindano hayo amesema mashindano hayo yameleta fursa kwa wafanyabiashara kukuza biashara zao .
“Nimefika kushiriki mbio hizi ili kuchangia uboreshaji miundo mbinu ya afya na elimu Mkoa wa Mbeya kama sehemu ya malengo na ndoto za Dkt.Tulia kuhakikisha eneo la afya na elimu inakuwa na ubora,”amesema.

More Stories
Ngozi:Wanawake nchini wanakila sababu ya kumshukuru Rais Samia kutoa nafasi za uongozi kwao
Wataalamu wa ujenzi mfumo wa NeST wanolewa usalama wa mifumo
Prof.Muhongo amshukuru Rais Samia kwa fedha nyingi miradi ya elimu Musoma Vijijini