May 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu Wenye Ulemavu wamchangia Samia Milioni 1 kwa ajili ya Fomu ya Urais

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameshiriki Kongamano la watu wenye ulemavu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar lililoandaliwa na Ikupa Trust Fund kama mgeni rasmi akimuakilisha Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko naibu waziri mkuu na waziri wa nishati, kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar, Dodoma Mei 09,2025,

Kupitia kongamano hilo Ridhiwani amewahakikishia Washiriki utayari wa serikali kushirikiana nao katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kushiriki shughuli zote za kijamaa ikiwemo kujenga uchumi na kujenga Jamii itakayopambana kwa ajili ya maslahi mapana ya Wenye Ulemavu,

Katika hatua nyingine Kikwete amepokea mchango wa Tsh milioni moja kutoka kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya uchukuzi wa fomu ya kugombea urais ya. Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu unaotajiwa kufanyika mwaka huu.

Kikwete amekabidhi vifaa wezeshi kwa makundi hayo ya watu wenye ulemavu, mafuta chupa 103 ya tshs 2,060,000/= , Miwani ya jua 38 ya tshs 190,000/=, Magongo 91 ya thamani 4,550,000/=, Fimbo nyeupe kwa wasioona 36 za tshs 1,260,000/=, Kofia 27 za tshs 405,000/=, ambavyo vyote vina zaidi ya thamani ya shilingi milioni nane.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kikwete amewakumbusha Watu wenye Ulemavu kuwa nao ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo sawa na wasio na ulemavu na hii ndiyo imekuwa dhamira ya Rais wa wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan.