Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Nyasa Mhandisi Stellah Manyanya amesema mamba waliozagaa Ziwa Nyasa na Mto Mbawa wanakuwa kikwazo katika eneo la utalii nchini.
Aidha Mbunge huyo amehoji kuhusu kifuta machozi kwa familia tatu ikiwemo ya Lundo,Kingerikiti na Lipingu ambao wapendwa wao walikamatwa na mamba katika Ziwa Nyasa na Mto Mbawa.
Mhandisi Manyanya ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi Cha maswali na majibu.
“Pamoja na kuwakumbusha Wizara kuhusu kifuta machozi kwa familia tatu ya Lundo,Kingerikiti na Lipingu ambao wapendwa wao walikamatwa na mamba Ziwa Nyasa na mto mbawa,
“Je kutokana na matukio hayo kuwa mengi na mamba wamekuwa wakizagaazagaa kwenye Ziwa Nyasa ambalo tunatamgaza utalii linakuwa tishio kwa watalii ,lini serikali itafanya maamuzi madhubuti ya kuwavuna mamba hao ikizingatiwa kuwa hata ngozi yao ni biashara kubwa.”alihoji Mhandisi Manyanya
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Maliasili Danstan Kitandula amekiri kuwasiliana na Mbunge huyo kuhusu mashambulizi ya mamba kwa familia hizo tatu .
Aidha amesema tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwamba wataalam wa TAWA kupeleka timu kwenye eneo hilo kwenda kufanya tathimini ya uhalali wa malipo yao na kuweka mikakati ya kuwavuna mambo katika eneo husika.
More Stories
RMO,DMO waagizwa kumsimamia Mkurugenzi ununuzi vifaa ,vifaa tiba
Mgogoro wa mipaka Ushetu,Kaliua watua Bungeni
Serikali ya nunua hereni za kidijitali kwajili ng’ombe,mbuzi na kondoo