May 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo:DMDP kujenga barabara za urefu km 67 Ilala

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Ilala

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo,amesema mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji( DMDP) awamu ya pili unatarajia kujenga Barabara za urefu km 67 Wilayani Ilala ,barabara hizo za kisasa zitawekwa lami na kufungwa taa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo Mei 3,2025 Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo,amesema mradi huo  wa DMDP ukikamilika utatatua sehemu ya changamoto katika baarabara ambazo zimekuwa kero maeneo tofauti .

“Mradi wa awamu ya pili wa DMDP   barabara za urefu wa KM 67 utakomboa wilaya ya Ilala itakuwa ya kisasa kama ulaya ndogo jiji letu litapendeza, tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ambapo ndani ya wilaya yetu hizi barabara zitakuwa mkombozi kwa wananchi mradi ukikamilika.

Ametaja moja ya  barabara zinazojengwa kwa lami katika mradi wa DMDP Kitunda_ Kivule njia nne kwa sasa Mkandarasi wa Mradi wa DMDP yupo kazini na maeneo yenye changamoto ya mashimo atayaboresha  .

Aidha amesema barabara ya Kimanga-Mazda ina urefu wa  km 3 itajengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025   na Halmashauri ya jiji  la Dar es Salaam na TARURA ambapo itajengwa kwa kiwango cha lami  mita 500 na zege katika daraja la Kimanga.

Vilevile amesema barabara korofi za Tabata-Kimanga mpango wa kuzifanyia matengezo katika mashimo umekamilika na baada mvua Mkandarasi atamalizia .

Ametaja barabara zingine zitakazojengwa kwa kiwango cha lami kuwa ni Pugu Majohe -mbondole njia nne ina urefu wa Kilometa 12.6 inafanyiwa usanifu itajengwa kwa kiwango cha lami katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 na eneo la halisi Kata ya Majohe itajengwa kwa kiwango cha Zege mita 400 na eneo litakalobaki litakarabatiwa kwa kiwango cha changarawe.