May 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uhakiki na uchambuzi wa kazi za waandishi wa tuzo za Samia Award wafanyika kwa weledi

Na Bakari Lulela,Timesmajira

MCHAKATO wa uhakiki na uchambuzi wa kazi za waandishi wa habari walioshindania kalamu awards 2025 uliofanyika kwa weledi katika kuwapata washindi wa tuzo hizio.

Akizungumza na waandishi wa habari Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt. Egbert Mkoko amesema tuzo hizo zinalenga kutambua na kuhamasisha waandishi wa habari wa kitanzania.

“Majaji tulikuwa 8 na tulipokea ujumla ya kazi1,131 kutoka kwa washiriki mbalimbali wakiwemo watayarishaji wa vipindi, waandishi wa habari wa Redio, televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii pamoja na maafisa habari kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi,” amesema Mkoko

Aidha Mkoko ameeleeza kuwa ushiriki huu mkubwa ni ushahidi wa mwitikio chanya wa wadau wa habari nchini katika kuezi uandishi wa habari za maendeleo.

Hata hivyo mchanganuo wa kazi zilizowasilishwa ni 263 kutoka magazetini, kazi 302 kutoka Redio , kazi 275 kutoka kutoka televisheni na kazi 291 kutoka kwa waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti waliowasilisha kazi zao njia mbalimbali za wasiliano.

Mchakato wa tathmini uliongozwa kwa misingi ya hali, weledi , uwazi na uadilifu pamoja na vigezo ikiwemo ulinganifu wa kazi na mada za maendeleo, ubora wa uandishi na matumizi ya lugha , utafiti na uchambuzi wa kina ,ushawishi na matokeo.

Aliendelea uzingatiaji wa maadili ya taaluma , Uraia, lugha ya uchapishaji, uadilifu binafsi, mapokeo kwa hadhira, matokeo chanya ya makala ambapo Makala inatakiwa iwe imechangia katika kuleta mabadiliko.