April 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Buhigwe aomba wataalam wa mionzi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MBUNGE wa Buhigwe Eliadon Kavejuru ameiomba Serikali kupeleka wataalam wa Afya katika wilaya ya Buhigwe ambayo ina miundombinu na vifaa vya kisasa katika Vituo vya Afya na Hospitali ya wilaya lakini hakuna watumishi wa Afya huku

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2025/2026,Mbunge huyo amesema licha ya mafanikio yaliyopo lakini bado wanakabiliwa changamoto mbalimbali katika Vituo vya Afya na Hospitali ikiwemo ya kukosekana kwa wataalam wa X-RAY na Ultrasound.

“Tuna changamoto katika Hospitali ya wilaya ya Buhigwe ,hatuna wataalam lakini katika Vituo vya Afya tuna X-RAY mbili ,Ultrasound nne lakini hakuna mtaalam hata mmoja.”alisema na kuongeza kuwa,

“Tunaomba tupatiwe wataalam wa mionzi Ili vifaa hivyo vitoe huduma katika wilaya yetu.”

Vile vile ameserma wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za watumishi wa Afya na ustawi wa jamii wapatao 476 huku akiomba katika ajira zitakazotolewa wapate watumishi hao.

Kuhusu sekta ya Elimu alisema,wamepata miradi mkubwa mikubwa ndani ya miaka mitano ambapo shule Saba za sekondari zimejengwa lakini pia wamepata fedha za ujenzi wa madarasa ya shule za msingi.

Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo bado Wana upungufu wa watumishi Idara ya Elimu wapatao 1,144 .

Katika hatua nyingine Mbunge huyo ameiomba Serikali iweke kipaumbele katika kukarabati shule kongwe za msingi ambazo zina zaidi ya miaka 50 huku akisema shule hizo zimechakaa sana huku akizitaja shule hizo kuwa ni pamoja na Muhinda,Kivande,Nyamagala,akitambuka na Nyamgali.

Akizitaja shule nyingine kongwe zinazohitaji ukarabati kuwa ni Nyakimwe,Kinungu,Msagala,Mwayaya ,Nyarugoza,Songambele,Mbanga,Kajana,Mlela na Katundu.