Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Mbulu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Askofu Dkt. Alex Malasusa amezindua jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Rufaa ya Kilutheri ya Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara, lenye thamani ya bil.6.5.
Uzinduzi huo umefanyika kwenye madhimisho ya Jubilee ya miaka 70 ya hospitali hiyo,ambapo Dkt. Malasusa amesema hospitali hiyo ina mchango katika kulihudumia Taifa kwani inahudumia wananchi kutoka Wilaya 7 na mikoa 4.
“Hospitali yetu hii ya Haydom imeendelea kuboresha miundombinu kwa kujenga jengo la Mama na Mtoto kubwa na la kisasa lililogharimu kiasi cha bilioni 6.5,”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tiba wa Hospitali ya Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara Dkt. Paschal Mdoe, amesema hospitali hiyo ilianzishwa mwaka 1955 ilikua na vitanda 50 hadi sasa wana vitanda 420 na ilipandishwa hadhi mwaka 2010 ambapo kwa mwaka inahudumia jumla ya wagonjwa 105,296 wa nje na 14,020 wa ndani.
More Stories
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi
Apps and Girls, Yas Waadhimisha Mahafali Wahitimu wa Jovia 2025