Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu,ameagiza Kamati za Siasa za chama hicho Wilaya ya Ilala, kuchagua na kupitisha wagombea wenye sifa, watakaosimama katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Mtemvu ,amesema hayo katika Futari Maalum kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Ilala futari iliandaliwa na chama hicho wilayani humo.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam,kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la Mpiga Kura ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (MNEC ) Simba Gadaf,amesema Kata 36 za Wilaya ya Ilala zitabakia CCM,hivyo itashika Wajumbe wa Halmashauri Kuu wahamasishe vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alitumia fursa hiyo kuwapa zawadi Wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa mapambano ya kutetea chama ikiwemo kusimamia na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.
More Stories
Akiba Commercial Benki yaweka tabasamu, kituo cha kulelea watoto Chakuwama Sinza
Wananchi Ikungi watakiwa kutumia mtandao kwa manufaa
UWT yalaani shambulio la kudhuru mwili Mwenezi BAWACHA