Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo , ameagiza miradi yote ya maendeleo wilayani humo,ikamilike kwa wakati ili wananchi waweze kufurahia matunda ya Serikali yao.
Mpogolo,amesema hayo katika ziara yake Kata ya Msongola ya kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi Jimbo la Ukonga,ambapo amesema ili miradi ya maendeleo ilete tija kwa wananchi,ametaja miradi viporo yote ikamilishwe.

“Nimepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kituo cha afya Mvuti wenye thamani ya milioni 500,pia ujenzi wa shule ya sekondari Kigezi Kata ya Buyuni na Yongwe Kata ya Chanika imefikia asilimia 90,hivyo ifikapo Aprili Mosi,mwaka huu shule hizo zianze kupokea wanafunzi,”amesema Mpogolo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar- es-Salaam Dkt.Zaituni Hamza ,amesema kituo cha afya Mvuti kimejengwa kwa thamani ya shilingi milioni 500 fedha zilizotolewa na Serikali katika miradi ya afya.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Yongwe Kata ya Chanika, Carl Chiwangu, ameeleza kuwa walipokea kiasi cha milioni 350, ambazo zimetumika kujenga madarasa 6, ofisi 2 , maabara na jengo la utawala pamoja na miumdombinu mingine.

More Stories
Dkt.Mpango azindua shule ya sekondari itakayojengwa na CRDB Dar
NBAA, ZIAAT wasaini hati ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja
Simbachawene:Tanzania,Afrika inahitaji viongozi wa kimageuzi katika kuhamasisha juhudi za pamoja