Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
Wananchi 75 wa Kata ya Kisukuru nimegawa wakiwemo wajumbe wa mashina wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),wamepatiwa bima za afya kwa ajili ya kuwasaidia kwenye matibabu pindi wanapopata magonjwa mbalimbali.
Bima hizo zimetolewa na Diwani wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome, lengo ni kusaidia wananchi na kuunga mkono Serikali katika kusaidia jamii kwenye suala la matibabu.
Sanjari na hayo,Lucy alitumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi na wajumbe wa mashina kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura,ili waweze kupata fursa kupiga kura katika uchaguzi Mkuu,ambapo zoezi hilo la uandikishaji mkoani Dar-es-Salaam limeanza Machi 17 mpaka 23 mwaka huu .
Hata hivyo amesema kwa Kata ya Kisukuru Serikali imefanya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za lami ,maji safi na salama, shule za msingi na sekondari pia inatarajia kujenga hospitali ya kisasa yenye hadhi ya Wilaya
More Stories
Ujenzi Maabara za masomo ya sayansi waendelea Musoma Vijijini
TBS:Majibu ya sampuli kutoka TBS yanaamika kokote duniani
Waziri Mkuu mgeni rasmi maadhimisho ya siku ya misitu Duniani