Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
TAASISI ya Tiba ya Mifupa,ubongo,mgongo na mishipa ya fahamu(MOI)imesema Katika kipindi cha miaka minne,imefanikiwa kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa 7,366 ambapo gharama za matibabu hayo ndani ya nchi zilikuwa Shilingi za Kitanzania bilioni 68,451,603,600.00 na kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 218,280,169,470 zingetumika.
Hivyo serikali imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 149,828,565,870.00 ambazo zimetumika katika shughuli nyingine za maendeleo.
Hayo yamesema jijini hapa leo,Machi 5,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhus mafanikio na muelekeo wa Taasisi hiyo katuka kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu sita.
Dkt.Ulisubisya amesema kuwa Katika kipindi cha tajwa Serikali imeiwezesha taasisi hiyo kuwa na vifaa vya kisasa ambavyo ni mashine za kisasa za zakupumulia (ICU Ventilators), Monitors, Vitanda na Ambulance ya kisasa (Vyenye thamani ya Tsh billion 1.3)
“Serikali imetoa Tsh Bilioni 4.4 kwajili ya ununuzi wa mashine mpya ya kisasa ya MRI na CT scan kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma hiyo kwa uhakika na wakati bila ya kusubiria huduma muda mrefu,”amesema.
Pamoja na miradi mingine Dkt.Ulisubisya amesema kuwa Mradi mwingine ni ujenzi wa ‘oxygen plant’ ambao umekamilika kwa asilimia 100% na gharama za mradi huu ni Tsh. 1,675,893,448.84 na utasaidia Taasisi ya MOI kuokoa Tsh. 1,150,000.00 kwa siku ambazo zilikua zinatumika kununua hewa ya Oxygen.
Aidha amesema kuwa ndani ya miaka minne Taasisi ya MOI imetekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi kupitia huduma za tiba mkoba katika hospitali mbalimbali zikiwemo Nyangao (Lindi), Hospitali ya Kanda ya kusini (Mtwara), Hospitali ya Mtakatifu Benedikt (Ndanda Mtwara), Hospitali ya Rufaa ya Nkinga (Tabora), Hospitali ya Mnazi Mmoja (Zanzibar) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambapo jumla ya wagonjwa 44,096 Walihudumiwa na wagonjwa 5,382 walifanyiwa upasuaji.
“Pia, Taasisi imesogeza huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi kupitia huduma ya kliniki Jongefu ya MOI (MOI Mobile clinic) ambapo huduma zimetolewa katika maeneo ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Gongo la mboto, Bagamoyo na Morogoro ambapo jumla ya wagonjwa 2,224 wamehudumiwa.
Pamoja na hayo ameelezea mipango ya baadae ya Taasisi hiyo kuwa ni kuendelea kuboresha huduma zao kwa viwango vya kimataifa,Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao (Rehabilitation centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji jijini Dar es salaam.
Kusogeza huduma katika jengo ambalo lilikua linatumika na Hospitali ya Tumaini upanga ili sehemu ya wagonjwa wa nje waanze kupata huduma katika jengo hilo na kupunguza msongamano MOI,Kuendelea kusogeza huduma zetu karibu na wananchi katika mikoa ambayo hatujaifikia (Tanga, Ruvuma, Kigoma,Geita, Njombe, Manyara, Mara na Kagera)
Pamoja na Kuanzisha huduma mpya za kibingwa na kibobezi ambazo hazipatikani hapa nchini kama vile ‘Bone Bank’ na matibabu ya ‘Parkinson’s disease’ na kutetemeka ndani ya miaka mitatu.



More Stories
Dkt.Biteko :Serikali kujenga mtandao mkubwa wa mabomba ya gesi
Walimu waaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu
Watoto yatima 100 wapatiwa bima za afya Rorya