March 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi:NBC yaunga mkono Serikali kidijitali

Na Mwandishi wetu , Timesmajira Online

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi Maryprisca Mahundi,amesema Benki ya Taifa ya Biashara(NBC),imeunga mkono Serikali sanjari kukuza uchumi jumuishi ndani na nje ya nchi kupitia hatua iliochukua ya maendeleo kidijitali.

Mhandisi Mahundi,amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa utoaji huduma kidijitali wa NBC,jijini Dar-es-Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Amesema,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inatambua jitihada zinazofanywa na NBC kuhakikisha inatoa huduma bora na haraka kwa wananchi.

Pia amesema, Serikali imepanua wigo kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ili kuongeza ufanisi kibiashara kwa njia ya kidijitali kitaifa na kimataifa kwa kutumia mkongo wa Taifa utakaofika kwenye mikoa yote nchini.