Na Penina MalundoTimesmajiraonline
MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo amesema Rais Samia Suluhu Hassan, tangu ameingia madarakani amefanya mambo makubwa mkoani Arusha, hasa katika Jimbo lake la Arusha Mjini.
Amesema jimbo la Arusha Mjini limepata mafanikio mbalimbali katika sekta ya maji, umeme pamoja ujenzi wa vituo vya afya ambavyo ujenzi wake umekamilika kwa wakati.
Pia alisema mbali na mafanikio hayo, wanawake wa jimbo la Arusha wamejipanga kumpokea Rais Samia katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 ambapo kitaifa yanatarajia kufanyika katika jimbo lake.
Akizungumza jana Mkoani Arusha ,Gambo alisema alichokifanya Rais Samia ni zaidi ya upendo kwa kwenda kwake mkoani humo kwenye maadhimisho hayo.
Alisema mtu akikuonesha upendo unapaswa kumuonesha mahaba, hivyo fursa hizo zinapokuja uwa zinachochea uchumi katika jimbo hilo.
”Yapo baadhi ya majimbo kiongozi akipita wakati wa kampeni kurudi kwake ni majaliwa,sisi hapa Dkt.Samia hakauki katika jimbo letu, kwa kweli kati majimbo yanayotakiwa yashindane 2025 kwa kumpa kura nyingi Rais Samia ni Jimbo la Arusha na Dodoma Mjini,” alisema.
”Kwa sababu hayo ni maeneo ambayo anaenda mara nyingi, tena wenzetu wa Dodoma wamepata bahati ya Kijiografia tu Makao Makuu yapo kule,Ikulu ipo kule…ila sisi huku anakuja kwa kwa sababu ya mahaba,”alisema.
Gambo alisema wananchi wa jimbo la Arusha mjini wanamshukuru Rais Samia kwa kuwaletea vitu vingi ikiwemo X-ray, Mashine ya CT Scan katika hospitali mbalimbali ikiwemo ya Mount Meru.
”Mimi kwa nafasi yangu ya ubunge mambo yangu yanaishia katika Jimbo hapa,wilaya na mikoa inawenyewe mimi nadeal na kata 25 hizi na mitaa 154.
”Hapa nikitaka kwenda popote siombi kibali kwa sababu wana-Arusha walishanipa 2020 na sanasana nisipokwenda watanishangaa mbona mbunge hatumuoni kwa sababu ni wajibu wangu kwenda kwao,”alisisitiza.
Alisema wanaposema Mama Samia miaka mitano tena, wanasema kwa sababu wanamambo wanayoishi katika Jimbo lao la Arusha.
More Stories
Rais Samia aridhishwa na utekelezaji miradi Tanga
Ziara ya Rais Samia yaanza kwa kishindo mkoani Tanga
Samia ajitosa madai yawalimu wasio na ajira