Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
CHAMA cha National League for Democracy (NLD) chajiweka vizuri kukabiliana na vyama vingine katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho, Tandika jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa NLD,Doyo Hassan Doyo,ameeleza hatua zinazochukuliwa na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu,ambapo kimeanza kufanya vikao mbalimbali vya tathmini ya uchaguzi uliopita, hususani wa Serikali za Mitaa, vijiji, na vitongoji.
Pamoja na kukutana na changamoto katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji, na vitongoji,Doyo amesisitiza kuwa hilo halitakuwa kikwazo kwa chama hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu.Â
 “Kwa wale ambao wana sababu za kususa, na wasuse, lakini NLD,hakiwezi kumuachia nguruwe shamba la mihogo,tutashiriki uchaguzi mkuu kwa kiwango kile kile mpaka dunia ijuwe kwamba haki yetu inapokonywa hapa,”amesema Doyo
Chama cha NLD kimeendelea na vikao vya kikanuni, lengo likiwa ni kupata wagombea wanaokubalika katika jamii kwa ajili ya nafasi za Ubunge, Urais, na Udiwani.
Â
More Stories
Polisi kuchunguza madai ya mwanafunzi kutupa kichanga chooni
Sekiboko ahimiza uwekezaji Elimu ya ufundi
Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti