Na Allan Kitwe, TimesMajira Online, Tabora
VIONGOZI na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora wamepongeza uimara wa Chama hicho tangu kuanzishwa kwake na kubainisha kuwa umechochewa kwa asilimia 100 na uimara wa Viongozi wake kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa.
Wakiongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwenye maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM wamesema kuwa uimara wa Viongozi wa CCM ndio mtaji mkubwa wa chama hicho kuendelea kuaminiwa na wananchi kushika dola hapa nchini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Said Juma Nkumba ameeleza kuwa tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977 CCM imeendelea kuthibitisha kuwa ni chama bora na chenye uwezo mkubwa wa kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Amesisitiza sifa kubwa ya chama hicho kuwa ni uimara wa Viongozi wake kuanzia ngazi ya juu hadi chini, hali ambayo inakifanya kutoyumbishwa na mtu mmoja au kikundi fulani cha watu wenye maslahi binafsi.
Sifa nyingine ambayo imekibebea chama hicho ni umoja na mshikamano wa viongozi na wanachama wake kuanzia ngazi ya mashina hadi taifa, kuandaa makada ambao watapokea kijiti cha uongozi na kuendelea kudumisha demokrasia,
Katibu wa CCM wa Mkoa huo Wilson Nkambaku amedokeza siri ya chama hicho kuendelea kuwa chaguo namba 1 la watanzania katika chaguzi zote ni uimara wa viongozi wake na uwezo wa kusimamia utekelezaji ilani yake ya uchaguzi.
Amebainisha kuwa CCM imeendelea kutimiza malengo yake ya kuwaunganisha wananchi wote na kuwatumikia kwa weledi mkubwa pasipo kuangalia itikadi zao za kisiasa ikiwemo kujenga mahusiano mazuri na vyama rafiki vya nchi nyingine.
‘Tunajivunia kuwa na viongozi makini na wenye maono makubwa ya kimaendeleo, hii ndio CCM inayopendwa na watanzania, na itaendelea kuaminiwa, nashauri wenzetu wa upinzani waendelee kujifunza ili wajenge vyama vyao’, amesema.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa huo Idd Moshi ametaja sababu kubwa ambayo inakifanya chama hicho kuendelea kukaa madarakani tangu kizaliwe ni kwa sababu kiko karibu zaidi na wananchi wake na kinajali sana maslahi yao.
Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa chaguo namba 1la wananchi kutokana na mkakati wake wa kuhakikisha kero zao zinatatuliwa kwa wakati na kuhakikisha yale yote yaliyoelezwa katika ilani yake ya uchaguzi yanatekelezwa kwa vitendo.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-1024x768.png)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-2-1024x768.png)
More Stories
Dkt.Mpango aagiza mfumo wa NeST utumike kudhibiti ubadhirifu,aipongeza PPRA
Mpogolo ashauri Ilala kutenga bajeti ya mazingira
DC Malisa ataka taarifa mahudhurio ya wanafunzi