February 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NMB yahudhuria Mkutano wa CSSC

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Uwakilishi wa Benki ya NMB ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna umehudhuria Mkutano wa Kamisheni ya Huduma za Kijamii ya Kikristo (CSSC), mkutano unaoangazia masuala ya elimu na afya. Mkutano huu unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.

Benki ya NMB imekuwa na ushirikiano mzuri na Kamisheni hii ambapo baadhi ya mashule na hospitali zao zimekuwa zikitumia mifumo ya Benki ya NMB ya kidijitali inayorahisisha ukusanyaji wa Sadaka, ulipaji bili za huduma za afya na uchangiaji wa miradi mbalimbali. Zaidi, mifumo hii imesaidia kupunguza upotevu wa mapato, kupunguza gharama kubwa za uendeshaji, kuonyesha uwazi, usimamizi wa miamala (yaani reconciliation) na kufanya malipo mbalimbali kwa wakati.

Mkutano huu umeongonzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Huduma za Kijamii ya Kikristo, Ndg. Peter Maduki na kuhudhuriwa na Maaskofu wote nchini.

NMBKaribuYako