![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG_20250210_133811_2152-1024x619.jpg)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG_20250210_133608_1712-1024x985.jpg)
Na Joyce Kasiki,Timesmajira Dodoma
BAADHI ya watumishi Kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamefanya ziara ya Mafunzo Tanzania Bara kufuatia agizo la Rais wa Serikali hiyo Dkt.Hussein Ally Mwinyi, kwa ajili ya kujifunza namna ya utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Malezi,Makuzi ,na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM 2021/22-2025/26) ilivyofanikiwa tangu mchakato wa uanzishwaji wake hadi utekelezaji wake unaotarajiwa kukamilika mwakani .
Ugeni huo umetembelea ofisi zinazoratibu kazi za Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) Tanzania Bara ikiwemo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kisha Ofisi ya Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN ) ambao wanafanya Uratibu katika utekelezaji wa PJT-MMMAM.
Akizungumza mara baada ya majadiliano na watumishi wa TECDEN ,na baadhi ya wajumbe wa timu ya utekelezaji wa PJT-MMMAM mkoa wa Dodoma,Dkt.Ibrahim Kambole Kutoka Taasisi ya ufuatiliaji na Usimamizi Utendaji Serikalini ,Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar amesema,ziara yao ni ya siku tatu na anaamini baada ya ziara hiyo watakwenda kufanya vizuri kutokana na waliyojifunza.
“Tupo Dodoma kwa Ziara ya siku tatu kwa ajili ya kujifunza wenzetu wamewezaje kuanzisha mpka kufikia utekelezaji wa PJT-MMMAM ambayo inaelekea mwishoni katika utekelezaji wake,
“Hivyo tumetembelea ofisi zinazoratibu kazi za MMMAM Tanzania Bara, sisi Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais Ikulu tunafanya kazi ya kuratibu uanzishaji au uimarishaji miradi ya programu za Malezi, Matunzo na Usalama na Elimu ya awali kwa watoto.”amesema Dkt Ibrahim
Aidha amesema,programu hiyo kwa Zanzibar , imewekewa mkazi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi mwenyewe ambapo kwa kuamua hivyo ameona umuhimu wa kuhakikisha watoto wapo salama, wanapata mazingira wezeshi , wanapata lishe Bora pia Wana usalama kama watoto.
“Kama tunavyoelewa mtoto akizaliwa katika mazingira wezeshi ,akilindwa, kulelewa na kupata Elimu ya awali nzuri atakuwa na mwisho mwema na atafanya vizuri katika masomo ,atakuwa mtu anayejielewa na hii ndiyo rasimali ya kusimamia katika Nchi yetu”amesema Dkt.Ibrahim na kuongeza kuwa
“Rais ametuagiza kama Taasisi tuhakikishe tunaratibu hili jambo ili i tupate mafanikio kwa haraka zaidi.”
maeneo yaliyotembelewa na Ugeni huo kwa ajili ya kuona mazingira na kujifunza ni pamoja na Makao ya Watoto Kikombo jijini Dodoma.
“Tumefurahi na tuneoata vitu vingi hasa katika majadiliano wenzetu wa TECDEN pamoja na watendaji wengine wa Programu wametupa vitu vingi tangu Mwanzo mpaka ilipofikia sasa na ipo mahali pazuri,
“Tunaendelea kujifunza na bila shaka tukirudi Zanzibar itakuwa ni chachu ya kusaidia na sisi kuendelea kusimamia agizo la Rais”
Awali Bruno Ghumpi Kutoka TECDEN alieleza mbele ya ugeni huo tangu majadiliano ya awali kuhusu Malezi ya watoto wadogo yaliyoanza tangu mwaka 2004,kusuasua kwake na hatimaye Wadau wakiongozwa na TECDEN kuanzisha tena mazungumzo hayo mwaka 2018 kuhusu uwepo wa Programu itakayoweka mustakabali wa watoto wadogo kwa maslahi mapana ya Taifa na hatimaye PJT-MMMAM nayolenga watoto wenye umri wa 0 hadi miaka 8 kuzinduliwa 2021.
More Stories
Wasira:Uchaguzi Mkuu utafanyika wanaCCM,Wananchi jiandaeni
Katavi yazindua mkakati wa kupambana na udumavu
RPC Kuzaga ahimiza matumizi sahihi ya silaha