Na Joyce Kasiki,Dodoma
WAZIRI wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ameitaka jamii kuona umuhimu wa kuhamasisha wanawake na wasichana kujiingiza katika fani za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ili kundi hilo liendelee kutoa mchango mkubwa kwa Taifa katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii hapa nchini.
Kikwete ameyasema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo alisema kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya 2022 kundi la wanawake na wasichana ni asilimia 51.3 na kwamba kiwango Cha kundi Hilo kinachoshiriki katika nyanja hizo ni asilimia 33 pekee.
“Hapa nchini Tanzania ,kiwango Cha kundi hilo kinachoashiria kazi za Sayansi Teknolojia na Hisabati kinakadiriwa kufikia asilimia 36.xalisema Kikwete
Alisema kutokana na ushiriki wao mdogo Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania zinatekeleza juhufi zake zinazolenga kuweka mazingira wezeshi ya kummotisha msichana na mwanamke .
Alisema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha usawa wa kijinsia katika sekta hizi, ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za elimu na mafunzo kwa wanawake na wasichana.
Aidha, alikumbusha umuhimu wa kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika sayansi, ikiwa ni pamoja na upungufu wa miundombinu, ukosefu wa vifaa vya kisasa na changamoto za kifedha ambapo alisema kuwa mazingira rafiki na wezeshi yajengwe ili kuwezesha wanawake na wasichana kujifunza bila vikwanzo.
Aidha alisema kwa kutambua nafasi na uwezo mkubwa wa wanawake na wasichana katika Sayansi na maendeleo ya kijamii,kiuchumi kwa ujumla Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo na sekta Binafsi ,zinaendelea kuchukua hatua za kuongeza ushiriki na mchango wa kundi la wanawake na wasichana .
Ametaja baadhi ya maeneo na juhufi mbalimbali zinazofanyika kuongeza ushiriki wa kundi Hilo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 sambamba na mitaala iliyoboreshwa ambapo Serikali imeanza msukumo mkubwa katika kuandaa walimu Bora ,kuwekeza katika mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia likiwemo kundi la wanawake na wasichana.
Pia amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia iangalie ushindani uliopo na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ya 2014 Toleo la 2023,ijikite katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Vile vile Kikwete ametaka ushirikiano wa Sekta ya Umma na sekta binafsi katika kubuni njia na mikakati ya kuimarisha na kuratibu ufungamishaji wa mipango na programu zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika STEM na ngazi nyingine za kisayansi.
Vile vile amezitaka sekta hizo kufanya tafiti mahsusi zinazolenga kubainisha hali halisi ya idadi ya wanawake na wasichana wanaojiunga na STEM katika ngazi mbalimbali nchini katika kipindi kisichozidi miaka kumi.
Katika hatua nyingine amezitaka sekta Binafsi na sekta ya umma kuendesha programu kabambe baina ya sekta ya umma na sekta Binafsi zinazolenga kuleta Mapinduzi katika ushiriki wa michango ya wanawake na wasichana na kuanzisha Mifumo rafiki ya kuvutisha wanawake na wasichana kufanya vizuri katika STEM utafiti na ubunifu nchini.
Awali,Naibu Katika Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt.Charles Mahera alisema shule za wasichana zimejengwa katika mikoa yote nchini ambapo pamoja na mambo mengine pia zinalenga kuhamasisha wasichana wengi zaidi kujiunga na masomo ya Sayansi.
‘Katikankuhakikisha wasichana wengi zaidi wanajiingiza katika masomo ya Sayansi,Serikali imejenga shule za wasichana mikoa yote,shule hizi zina mchango mkubwa katika kuhamasisha wasichana kusoma masomo ya Sayansi
More Stories
Wasira:Uchaguzi Mkuu utafanyika wanaCCM,Wananchi jiandaeni
Rais Dkt.Mwinyi atuma wajumbe kujifunza utekelezaji wa PJT-MMMAM
Katavi yazindua mkakati wa kupambana na udumavu