Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jones amewataka wanafunzi kuacha kuogopa masomo ya sayansi na hesabu na kusema kwamba siyo magumu kama inavyoelezeka.
“Ninyi wanafunzi mnaosoma msiogope masomo ya Sayansi na Hesabu kwani ni masomo pekee ambayo yanafaa duniani kote hivyo hayabadiliki na unaweza kuyapata mahali popote na kukufanya kuajiliwa mahali popote kwani yanaendandana na Teknolojia ya sasa”ameeleza Mwenyekiti wa Bodi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jones Kilimbe, wakati wa Maadhimisho ya siku ya Usalama Mtandaoni 2025 yaliyofanyika Jijini Dodoma leo,Februari 11,2025 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walimu wa shule ya msingi,vyuo vya kati na vyuo vya elimu ya juu.
Pamoja na hayo amesema usalama wa matumizi ya mtandao na kuhimarishwa vyema kwa matumizi bora na yenye faida ni wazi kuwa amani ya Nchi na mtu binafusi itakuwepo kwa kiwango kikubwa.
Amesema kuwa ili kuwa na taifa lenye watu bora kimaadili na kiuchumi ni bora kutumia vyema mitandao kwa matumizi bora na yenye manufaa kwa jamii pamoja na taifa kwa ujumla.
Akiendelea kuzungumza na wadau mbalimbali wa matumizi ya mtandao amesema kuwa kwa sasa kuna urahisi mkubwa matumizi ya kimtandao pamoja na hasara kubwa iwapo mitandao itatumiwa vibaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka TCRA,John Dafa amesema kuwa siku ya usalama mtandaoni uadhimishwa jumanne ya pili ya mwezi Februari kila mwaka ambayo ni mpango wa kimataifa ulioanzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi na salama ya mtandao wa intaneti.
“Siku hii inasheherekewa takribani katika nchi 190 duniani,vilevile maadhimisho haya yanaunganisha mabilioni ya watu ulimwenguni kuhamasisha matumizi sahihi na salama mtandaoni nakuongeza uelewa kuhusu masuala ya mtambuka mtandaoni haya miongoni mwa fursa yanayotokana na matumizi hayo,
“Huu ni mwaka wa 21 toka mtandao huu uanzishwe tangu mkakati huu wa Safer Internet yanayokwenda na Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu “Jilinde wewe na uwapendao dhidi ya ulaghai uhalifu mtandaoni”amesema.
Dafa amesema Kauli mbiu hiyo inatukumbusha umuhimu wa kuongeza umakini kwa kutumia mitandao na mifumo ya teknolojia katika dhama hizi za taarifa(Information society)ambapo matumizi ya teknolojia yakumbana na changamoto za wingi wa uangalifu mtandaoni hawa wanatumia mbinu mbalimbali zikiwemo zinazovutia nakushawishi.
More Stories
Rais Dkt.Mwinyi atuma wajumbe kujifunza utekelezaji wa PJT-MMMAM
Katavi yazindua mkakati wa kupambana na udumavu
RPC Kuzaga ahimiza matumizi sahihi ya silaha