February 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakurugenzi wahimizwa kusimamia mfumo wa NeST

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAKISEMI) Mohamed Mchengerwa amewaagiza Wakurugenzi Nchini kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi ya Mfumo wa Kielektroniki wa ununuzi wa Umma (NeST) ili uwe na tija kwa maendeleo ya Taifa na wananchi kwa ujumla.

Mchengerwa ametoa agizo hilo katika kikao kazi kuhusu mfumo huo ambacho kimeandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) huku kikishirikisha Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri,Makatobi Tawala wa Mikoa ,Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi wa Mikoa na Halmashauri.

Mchengerwa amesema,katika kusimamia matumizi ya Mfumo huo pia ni lazima wakasimamie utekelezaji wa Sheria pamoja na kanuni zake .

“Nawaagiza Wakurugenzi mkasimamie matumizi sahihi ya Mfumo wa NeST na utekelezaji wa sheriabya manunuzi pamoja na kanuni zake.”amesema Mchengerwa

Aidha ,amewataka Wakurugenzi hao wasimamie utekelezaji wa miradi katika Halmashauri zao na ikamilike kwa wakati .

“Katika kutekeleza miradi hiyo,mkatumie fedha za miradi kwa namna iliyokusudiwa ,kama kuna majengo hamjayakamilisha ,mkayasimamie yakamilike,

“Rais katuheahimu katupa nafasi hizi ,ametuheshimisha ,amewaamini mnaweza kumsaidia,sasa msiiondoe imani yake kwenu kwa kutofanya kazi kikamilifu.”amesema Mchengerwa na kuongeza kuwa

“Wapo ambao miradi ya shule hamjayakamilisha,hamuitambui miradi kwa sababu hamuendi kuteimbelea ,tusisukumane,tufanye kazi kwa kujituma na kumtanguliza Mungu wakati tukiwatumikia watanzania.”

Awali Mkurugenzi wa PPRA Denis Simba amesema tangu kuanza kutumika kwa mfumo huo Julai 2023 zimepatikana zabuni zenye thamani ya zaidi Trilioni 12.

Ameitaja Halmashauri ya Kwimba ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya Mfumo huo ambapo ina Zabuni 2,065.

Aidha pamoja na mafanikio mengine amesema mfumo huo umesaidia kudhibiti ununuzi wa umma