February 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shaka:Serikali haitaacha kusimamia wajibu wake kwa wananchi

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

MKUU wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan haitaacha wala kukengeuka kusimamia wajibu wake kwa wananchi na kuhakikisha haki, amani, mshikamano na utulivu wa kitaifa hauvurugwi kwa kiashiria
chochote ovu, bila ustawi wa amani, vyombo vya kutoa maamuzi kutenda haki, utulivu na upendo

Akizungumza leo Mkoani Morogoro wilayani Kilosa katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini,Shaka amesema hakutakuwa na njia mbadala ya kuwapatia wananchi maendeleo ya kisekta ikiwemo kuimarisha
huduma za kijamii na tuamini kwamba jamii nayo haiko tayari kuishi kwa mashaka, hofu na wasiwasi .

Amesema watanzania ni waungwana hawataki na wala hawajazoe maisha ya mikiki mikiki na vishindo au matukio hatarishi,wanachokijua ni kuwaona viongozi
wao wakisimamia amani, mshikamano, umoja wa kitaifa na upendo.

“Maisha ya mshikemshike na vurugu viko mbali na utamaduni wetu wa Kitanzania hivyo katika nyakati zote sera na mipango ya nchi imejikita katika suala la msingi la kuhubiri amani na utaifa kwa kujali
utu, usawa na haki kwa kila binadamu bila kutazama dini, rangi au kabila.

“Tunayahimiza masuala hayo kwa kuwa bila ustawi wa umoja, amani na utulivu shime ya maendeleo itaporomoka,kabla ya
mungu hajashusha vitabu vyake vitukufu Zaburi,Taurat, Injili na Quraan yaaminika dunia yote iligubikwa na kiza cha dhulma lakini kutumwa kwa mitume yake ndipo mwanga wa haki ukaadhihirika
na kupinga vitendo vyote ambavyo kwa kiasi kikubwa vilikandamiza misingi ya haki, usawa na utawala shariaa,”amesema.

Aidha amesema ushiriki na ushirikishwaji wa
wananchi na vyombo vya kutoa Haki kuanzia ngazi za vijiji, uwajibikaji wa taasisi mbalimbali na muhimili wa
mahakama ni muhimu kwa wananchi wa Kilosa.

” Serikali ya Wilaya ya Kilosa itasimamia mambo tisa mliyoshauri kufanyika
katika kuboresha mfumo wa haki madai nchini ili kupunguza migogoro ikiwemo kuanzishwa kwa mabaraza vijijini yatakayosimamiwa na wazee wa mila ili kusuluhisha na kupunguza migogoro ya
wananchi, Uwepo na utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri
zinazosimamia matumizi bora ya ardhi,
Kuhamasisha usuluhishi wa migogoro kama njia mbadala ya
kutatua kesi kwa haraka na kwa gharama nafuu kabla na
baada ya kufunguliwa mahakamani.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushauriwa wawe na utamaduni wa kuwatumia wanasheria ili katika mashauri mahakamani au kwenye taasisi za usuluhishi ili kuepuka maswala ya kiufundi
yanayoweza kuwakumba wakati wa uendeshaji wa mashauri
yao,Kuboresha miundombinu na rasilimali za mahakama na taasisi
za haki madai,Kuendelea kupambana na rushwa na kuongeza uwazi katika
utoaji wa haki madai pamoja na Kuimarisha elimu ya sheria kwa wananchi ili wawe na uelewe
haki zao,”alisema.

Hata hivyo amewaomba wanasheria na mawakili wa kujitegemea kuangalia upya ukubwa wa gharama huduma za sheria kuwa kubwa wakati mwingine wananchi wanyoge wanashindwa kuzitumia wakati
wao ndio waathirika wakubwa migogoro.

Pia amehimiza ushirikiano kwa Taasisi za
kusimamia haki madai zinapaswa kufuatilia migogoro kwa kushirikiana na serikali kuanzia ngazi zote kabla ya madhara kutokea na wakati mwengine kupelekea
watu kupoteza maisha sambamba na vyombo vya kusimamia haki vinapaswa kushughulikia kwa wakati
malalamiko yanayofunguliwa
kuondosha malalamiko ya wananchi ya kesi
kuchukua muda mrefu.