Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Ilemela
Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,wametakiwa kujiandaa na ukomo wa ruzuku inatolewa na mpango huo.
Hayo yamebainishwa Februari 3,2025 na Mwezeshaji wa TASAF Kata ya Nyamanoro,Mbwana Lunga, wakati akizungumza na walengwa hao,ambapo amewataka wajiandae,itakapofika Septemba 30 mwaka huu ndio itakuwa mwisho wa ruzuku kwa walengwa walioandikishwa kuanzia mwaka 2021.Huku akisisitiza mpaka viongozi wa mitaa watakapo wapatia taarifa nyingine mpya zitakazoelekezwa na mpango.
Pia amewataka wanufaika wa mpango huo kuzingatia matumizi bora ya nishati kama sera ya nchi inavyotaka ili kuimarisha uchumi na kulinda afya zao dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wake Martha Kaloli ambae ni mnufaika wa TASAF kutoka Kata ya Nyamanoro,amesema mpango umemsaidia kujikwamua kiuchumi kwani ameweza kuanzisha miradi midogo midogo inayomsaidia kusomesha watoto, kulipia gharama za chakula na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Huku Joyce Peter kutoka Kata ya Ibungilo, amewahimiza walengwa wenzake kutumia vizuri fedha wanazozipata na mradi waweze na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
TASAF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,imeendelea kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini katika mitaa yote 171 na kwamba fedha zimekuwa zikiwasilishwa kwa walengwa mmoja mmoja huku miradi mbalimbali ikitekelezwa kupitia mpango huo kama barabara, shule na zahanati kwa lengo la kuwaondolea wananchi umasikini.
More Stories
Rais Samia kupokea Tuzo ya ”The Gates Goalkeepers Award”
Kapinga:Azma ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote
Shaka:Serikali haitaacha kusimamia wajibu wake kwa wananchi