January 31, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti UVCCM ataka wakandarasi kuwa na weledi ujenzi wa miradi

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

WAKANDARASI wanaojenga mradi wa Maji  Rujewa katika Programu ya Miji 28 ya Tanzania Bara wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili  mradi huo uweze kukamilika kwa wakati kutokana na uhitaji wa maji kwa jamii uliopo.

Akizungumza Januari 30,2025 ,mara baada ya kutembelea mradi wa maji uliopo eneo la Igomelo kata ya Igawa  wilayani Mbarali ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya kutimiza miaka 48 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Mbarali (UVCCM)Medson Mwambapa amesema kwamba chama hicho kimefika Katika mradi huo kujionea maendeleo ya ujenzi wa programu ya Miji 28 ya Tanzania Bara.

“Hii kazi mnayofanya ndugu zangu wakandarasi kumekuwa na  changamoto ya kutomaliza kwa wakati miradi mingi inayotekelezwa na serikali hivyo niwaombe huu mradi ukamilike kwa wakati “amesema .

Amesema kuwa  maji ni kitu muhimu kwa jamii na kusema kuwa mradi huo unaenda kunufaisha maeneo matatu ambayo ni Mji wa Rujewa ambapo watu 189,685 wanaenda kunufaika na mradi huo.

Aidha Mwamba amesema kwamba maeneo mengine ni Makambako 105,933 pamoja Wanging’ombe  227,936 ambayo ni sawa na watu 523,554.

“Ni kitu ambacho tunatakiwa kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kama vijana wa chama cha Mapinduzi tunajivunia sifa ya kusema kwanini tunatakiwa kupiga mitano ni kama hivi tunaomba maendeleo na vijana tunatakiwa kutembea kifua mbele”amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji  Rujewa(RUJUWASA) Mhandisi,Kudra Yasin amesema kuwa mradi huo unatarajia kuzalisha maji kiasi  cha mita za ujazo Mil.40, kwa siku  ambapo kwa Rujewa  mahitaji ni lita 15 milion ikiwa lita 25 milion  zitakuwa kwa ajili ya Wanging’ombe na Makambako.

Akielezea zaidi Mhandisi Yasin amesema vijiji na Miji itakayonufaika ni Mji wa Rujewa ikiwa ni pamoja na kata ya Ubaruku,Imalilo Songwe na Igava na kwamba mradi huo unatekelezwa kwa njia ya mkataba na kuisha kwa mradi huo  kutapelekea kuwa na asilimia 100, za  utoaji wa utoaji wa huduma kwa wakazi wa Rujewa na vitongohi vyake.

“Mradi huu unatekelezwa ba serikali ya watu wa India kupitia Benki ya EXIM , muda wa mradi ni miezi 32,”amesema.

Hata hivyo Mhandisi Yasin amesema kwamba kupatikana kwa huduma ya maji kwa saa 24, ikiwa ni pamoja na kufikia malengo ya ilanibya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2020  na 2025 ya kufikia asilimia 95 Mijini  na mpaka sasa mradi  huo utekelezaji wake ni asilimia 20.9 kwa Mji  Rujewa kwa ujumla ni asilimia 22 kwa Miji yote mitatu .

Mmoja wa wananchi wa kata ya Igawa  wilayani Mbarali ,Furaha Rajabu amesema kwamba kukamilika kwa mradi huo kutapunguza uhaba wa maji kwa wakazi wa Mji wa Rujewa na vijiji vyake kutokana na kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maji .